Go Back   Sekenke Forums. > Ukumbi wa Sekenke > Ukumbi wa Dini

Reply
 
Thread Tools Search this Thread Display Modes
Old 12-16-2006, 09:57 PM   #1
rashid43
Super Moderator
 
rashid43's Avatar
 
Join Date: Dec 2006
Posts: 4,037
Default 17.MAJINA YA PEPO NDANI YA QUR-ANI.

Janna ni neno la Kiarabu na kwa Kiswahili ni Pepo. Na imeitwa Janna kwa sababu asili ya neno hili limetokana na maana ya fichika au funikwa. Kwa mfano kizazi kimeitwa kwa Kiarabu Janiin, kwani kizazi kimefunikwa tumboni mwa mama yake. Na ameitwa kwa Kiarabu Jinni kwani Majini wote wamefichika hawaonekani na macho ya watu. Na mwehu ameitwa kwa Kiarabu majnuun kwa sababu akili yake imefichika. Na pia Janna imeitwa kwa maana nyingine Bustani kwa vile ndani yake imefunikwa na miti. Na Pepo ina sifa chungu nzima na majina mbalimbali kulingana na hizo sifa. Yafuatayo ni majina ya Pepo yaliyotajwa ndani ya Qurani kama ifuatavyo:

1.DAARAL MUQAAMA.
Jina la kwanza la Pepo limeitwa Daaral Muqaama kwa sababu ni mahali pa kukaa Waumini daima, hawahami hami kwenda kuishi pahala pengine. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Surat Faatir aya ya 35, “
الَّذِي أَحَلَّنَا دَارَ الْمُقَامَةِ مِنْ فَضْلِهِ لا يَمَسُّنَا فِيهَا نَصَبٌ وَلا يَمَسُّنَا فِيهَا لُغُوبٌ
Maana yake, “Ambaye kwa fadhila Zake ametuweka katika Daaral Muqaama (nyumba ya kukaa daima); humo haitugusi taabu wala humo haitugusi kuchoka.”

2.DAARUL SSALAAM.
Jina la pili la Pepo limeitwa Daarul Ssalaam kwa sababu ni nyumba ya salama kutokana na kila ubaya, misiba na udhia. Na ni ile nyumba ya Mwenyezi Mungu S.W.T. imetokana na jina Lake Ssalaam. Kaiita Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Suratil A`naam aya ya 127, “
لَهُمْ دَارُ السَّلامِ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَهُوَ وَلِيُّهُمْ بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Maana yake, “(Watu wema) watapata Daarul-Ssalaam (Nyumba ya salama) kwa Mola wao. Naye Ndiye mlinzi wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyatenda.”

3.MAQAAMIN AMIIN.
Jina la tatu la Pepo limeitwa Maqaamin Amiin kwa sababu ni mahali pa amani, amani ya kila ubaya, na watu wake siku zote watakuwa katika amani. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Muumin (Ghaafir) aya ya 39, “
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ
Maana yake, “Hakika wachaMungu watakuwa katika Maqaamin Amiin (mahali pa amani).”

4.JANNAATU `ADNI.
Jina la nne la Pepo limeitwa Jannaatu `Adni na jina hili lina maana moja kwa Pepo zote na maana yake hasa ni makao au mahali au maskani ya kukaa daima. Kaiita Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Suratir Raad aya ya 23, “
جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا وَمَنْ صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ…
Maana yake, “Pepo za Adni wataziingia wao (pamoja) na waliofanya wema miongoni mwa wazee wao na wake wao na kizazi chao.”

5.JANNAATUL MA-AWA.
Jina la tano la Pepo limeitwa Jannaatul Ma-awa kwa maana ya makao au mahali pa kufikia. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Surat Sajda aya ya 19, “
أَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ جَنَّاتُ الْمَأْوَى نُزُلا بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Maana yake, “Wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri watakuwa na Pepo za Ma-awa. Ni andao lao kwa yale waliokuwa wakiyatenda.”

6.JANNAATUL KHULD.
Jina la sita la Pepo limeitwa Jannaatul Khuld kwa sababu watu wake wataishi daima na milele. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat Furqaan ya ya 15, “
قُلْ أَذَلِكَ خَيْرٌ أَمْ جَنَّةُ الْخُلْدِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ كَانَتْ لَهُمْ جَزَاءً وَمَصِيرًا
Maana yake, “Jee, haya ni bora au Pepo ya Khuld (Pepo ya milele) ambayo wameahidiwa wachaMungu? Iwe kwao malipo (mazuri) na marejeo (ya kuahidiwa).”

7.JANNAATUL FIRDAWS.
Jina la saba la Pepo limeitwa Jannatul Firdaws. Kama alivyotufahamisha Mtume wetu S.A.W. kwamba Pepo ya Firdaws ni Pepo yenye daraja ya juu zaidi kuliko Pepo zote na akaongezea kusema wakati tukiomba tumuombe Mwenyezi Mungu S.W.T. atupe Pepo ya Firdaws. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika SuratiI Kahf aya ya 107, “
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلا

Maana yake, “Hakika walioamini na kufanya vitendo vizuri makazi yao yatakuwa hizo Pepo za Firdaws.” Katika Hadithi iliyopokelewa na Ubaada bin Saamit R.A.A. na kutolewa na Ttirmidhi, Mtume S.A.W. kasema kuhusu daraja ya Pepo ya Firdaws, “
فِي الْجَنَّةِ مِائَةُ دَرَجَةٍ ، مَا بَيْنَ كُلِّ دَرَجَتَيْنِ كَمَا بَيْنَ الأَرْضِ وَالسَّمَاءِ وَالْفِرْدَوْسُ أَعْلاهَا دَرَجَةً وَمِنْهَا تُفَجَّرُ أَنْهَارُ الْجَنَّةِ الأَرْبَعَةُ وَمِنْ فَوْقِهَا يَكُونُ الْعَرْشُ فَإِذَا سَأَلْتُمُ اللَّهَ فَسَلُوهُ الْفِرْدَوْسَ
Maana yake, “Hakika katika Pepo kuna daraja mia, baina ya kila daraja mbili (ukubwa wake) ni kama baina ya mbingu na ardhi. Na Firdaws ni daraja ya juu na humo inabubujika mito minne ya Peponi. Na juu yake ipo Arshi. Na mkimuomba Mwenyezi Mungu muombeni (Pepo ya) Firdaws.”

8.JANNAATIN NA`IIM.
Jina la nane la Pepo limeitwa Jannaatin Na`iim kwa maana ya aina za neema mbali mbali watakazoneemeshewa watu wake ambazo zinapatikana katika kila Pepo kama vile vyakula, vinywaji na mavazi. Na hili jina limetajwa na Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat Yuunus aya ya 9, “
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُمْ بِإِيمَانِهِمْ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهِمْ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ
Maana yake, “Hakika wale walioamini na kufanya vitendo vizuri, Mola wao atawaongoza kwa sababu ya imani yao waende katika Pepo. Itakuwa inapita mito mbele yao, katika hizo Pepo za Na`iim (Pepo za neema).”

9.MAQ`ADI SIDIQ.
Jina la tisa la Pepo limeitwa Maq`adi Sidiq kwa sababu humo kitakuwapo kila kinachohitajika katika makao ya haki. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Qamar aya ya 54 na ya 55, “
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَهَرٍ * فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ…
Maana yake, “Hakika wachaMungu watakuwa katika Mabustani na mito. Katika Maq`ad Sidiq (makao ya haki)...”

10.DAARAL HAYAWAAN.
Jina la kumi la Pepo limeitwa Daaral Hayawaan kwa sababu humo ndiyo marejeo ya mwisho kwa waja wema, maisha yake hayana kikomo ni maisha ya kudumu milele. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Ankabuut aya ya 64, “
وَإِنَّ الدَّارَ الآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ
Maana yake, “Na nyumba ya Akhera ndiyo maisha hasa.”

Last edited by rashid43; 04-03-2012 at 07:17 AM.
rashid43 is offline   Reply With Quote
Old 11-09-2008, 12:59 AM   #2
Mordiy
Master
 
Mordiy's Avatar
 
Join Date: Oct 2008
Posts: 1,288
Default

Shukran Sheikh Rashid43 kwa post yako hii
__________________
Engineer Muhammad Saleh Bin-3ubadiy
Mordiy is offline   Reply With Quote
Reply

Thread Tools Search this Thread
Search this Thread:

Advanced Search
Display Modes

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off

Forum Jump

Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
KUIFAHAMU PEPO. rashid43 Ukumbi wa Dini 1 01-09-2010 11:57 AM
KUBASHIRIWA PEPO. rashid43 Ukumbi wa Dini 14 08-19-2009 02:31 PM
PEPO Mordiy Ukumbi wa Dini 1 12-08-2008 11:08 AM
25.MAJINA YA MILANGO YA MOTONI NDANI YA QUR-ANI. rashid43 Ukumbi wa Dini 1 11-09-2008 12:58 AM
Pepo!! ibrahim Mashairi, hekima au methali 1 11-05-2008 11:57 PM


All times are GMT +4. The time now is 07:06 AM.

Powered by vBulletin® Version 3.8.3
Copyright ©2000 - 2016, Jelsoft Enterprises Ltd. Mahmoud Al-Asmi