Go Back   Sekenke Forums. > Ukumbi wa Sekenke > Afya na tiba

Reply
 
Thread Tools Search this Thread Display Modes
Old 08-18-2011, 01:13 PM   #1
Zainab
Expert Member
 
Zainab's Avatar
 
Join Date: Aug 2011
Posts: 42
Default UGONJWA WA WASIWASI

Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuh.
Tatizo nililo nalo ni kubwa na la muda mrefu, hivyo atakayeweza kunifanya nipate nafuu katika tatizo langu hili hakika shukrani zangu kwake hazitakuwa na kipimo, na thawabu nyingi zitamfikia kwani kwa niaba ya Allah SWT, atakuwa ameniponya.

Mimi nina tatizo la ugonjwa wa WASIWASI. Wasiwasi huo umeniletea athari zifuatazo:
1. Siwezi kuongea katika kadamnasi (mkusanyiko) ya watu wengi hata kama ya kuongea ninayo. Moyo hunienda mbio, na pumzi kuziba.
2. Ninapopata taarifa mbaya hata kama hazina uzito sana, na wengine huzichukulia za kawaida mimi huziona kubwa, hukosa raha kabisa, hata chakula kinanishinda kula.
3. Ni nadra kunikuta nacheka na kufurahi.
4. Nikisikia jambo lazima nilifuatilie sana hata kama halina ulazima sikubali mpaka niujui mwisho wake.

Yote haya yamenifanya nipate vidonda vya tumbo (ulcers).

Tusaidiane Waislamu, nina hofu nisijepatwa na ugonjwa wa moyo kutokana na wasiwasi huu. Nimeshatumia dawa za ulcers na kuandikiwa makombe, lakini wasiwasi bado haunitoki, saa zote roho juu juu hadi mambo mengine ndugu zangu wananificha.

Nategemea busara zenu.

Last edited by Zainab; 08-23-2011 at 01:01 PM.
Zainab is offline   Reply With Quote
Old 08-18-2011, 05:59 PM   #2
rashid43
Super Moderator
 
rashid43's Avatar
 
Join Date: Dec 2006
Posts: 4,037
Default

Wa`alaikum Msalam Waarahmatullahi Wabarakaatuh,

Kwanza pole sana kwa ugonjwa uliokuwa nao kwa muda mrefu. Lakini hata hivyo usikate tamaa, bali endelea kumtegea Mola wako na kusoma dua. Insha-allah Mwenyezi Mungu atakupa shifaa.

1-Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi iliyotolewa na Ahmad, “Atakaepatwa na dhiki au huzuni au ukiwa aombe dua hii ifuatayo, “
‘‘اللَّهُمَّ إِنِّي عَبْدُكَ ، وَابْنُ عَبْدِكَ ، وَابْنُ أَمَتِكَ في قبضتك . نَاصِيَتِي بِيَدِكَ . مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤُكَ ، أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ ، أَوْ أَنْزَلْتَهُ فِي كِتَابِكَ أَوِ اسْتَأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ ، أَنْ تَجْعَلَ الْقُرْآنَ رَبِيعَ قَلْبِي ، وَنُورَ صَدْرِي ، وَجِلاءَ حُزْنِي وَذَهَابَ هَمِّي’’
“ALLAAHUMMA INNIY `ABDUKA WABNU `ABDIKA WABNU AMATIKA FIY KABDHATIKA. NAASIYATIY BIYADIKA. MAADHIN FIYYA HUKMUKA `ADLUN FIYYA QADHAA-UKA AS-ALUKA BIKULLI SMIN HUWA LAKA SAMMAYTA BIHI NAFSAKA AU `ALAMTAHU AHADAN MIN KHALQIKA AU ANZALTAHU FIY KITAABIKA AU STA-ATHARTA BIHI FIY `ILMI L-GHAYBI `INDAKA AN TAJ`ALAL QUR-AANA RABIY`A QALBIY WANUWRA SADRIY WAJILAA-A HUZNIY WADHAHAABA HAMMIY.”

Maana yake, “Ewe Mwenyezi Mungu! Hakika mimi ni mtumwa Wako, mtoto wa mtumwa Wako, mtoto wa kijakazi Wako, utosi wangu uko mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni usawa kwangu kunihukumu Kwako, nakuomba kwa kila jina ambalo ni Lako ulilojiita kwalo Mwenyewe, au uliloteremsha katika Kitabu Chako, au ulilomfundisha yeyote yule kati ya viumbe Wako, au ulilolihifadhi Wewe Mwenyewe, katika elimu iliyofichika Kwako, nakuomba uijaalie Qurani kuwa niraha na uchanuzi wa roho yangu na nuru ya kifua changu, na utatuzi wa huzuni yangu, na sababu ya kuondoka majonzi yangu.”


2-Pengine inahusu na mambo ya kijicho.

Bibi Aisha R.A.A.H. kasema katika Hadithi iliyotolewa na L-Bukhari, “
‘‘كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرَأَ فِيهِمَا قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ وَ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلاثَ مَرَّاتٍ’’
Maana yake, “Alikuwa (Mtume S.A.W.) akienda kulala kila usiku huiweka pamoja mikono yake kisha huipuliza akaisomea Qul-Huwa Llaahu Ahad na Qul-Audhu Birabbi L-Falaq na Qul-Audhu Birabbi Nnaas. Baadaye huipangusia mwilini mwake kwa kadiri ya uwezo na huanzia kichwani kwake na usoni mwake na iliyo karibu na mwili wake. Hufanya hivyo mara tatu.”


rashid43 is offline   Reply With Quote
Old 08-18-2011, 06:11 PM   #3
abjad
Master
 
abjad's Avatar
 
Join Date: Mar 2011
Posts: 2,998
Default

Quote:
Originally Posted by Zainab View Post
Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuh.
Tatizo nililo nalo ni kubwa na la muda mrefu, hivyo atakayeweza kunifanya nipate nafuu katika tatizo langu hili hakika shukrani zangu kwake hazitakuwa na kipimo, na thawabu nyingi zitamfikia kwani kwa niaba ya Allah SW, atakuwa ameniponya.

Mimi nina tatizo la ugonjwa wa WASIWASI. Wasiwasi huo umeniletea athari zifuatazo:
1. Siwezi kuongea katika kadamnasi (mkusanyiko) ya watu wengi hata kama ya kuongea ninayo. Moyo hunienda mbio, na pumzi kuziba.
2. Ninapopata taarifa mbaya hata kama hazina uzito sana, na wengine huzichukulia za kawaida mimi huziona kubwa, hukosa raha kabisa, hata chakula kinanishinda kula.
3. Ni nadra kunikuta nacheka na kufurahi.
4. Nikisikia jambo lazima nilifuatilie sana hata kama halina ulazima sikubali mpaka niujui mwisho wake.

Yote haya yamenifanya nipate vidonda vya tumbo (ulcers).

Tusaidiane Waislamu, nina hofu nisijepatwa na ugonjwa wa moyo kutokana na wasiwasi huu. Nimeshatumia dawa za ulcers na kuandikiwa makombe, lakini wasiwasi bado haunitoki, saa zote roho juu juu hadi mambo mengine ndugu zangu wananificha.

Nategemea busara zenu.
Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuh

Bismilahi Rahmani Rahiim

255. Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilio katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu


Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini
yake?


(hapana.......)

[line]-[/line]

ningependa unisaidie ili nami nipate alau kuchanga japo kdiiigi:

Jee hayo yaliokusibu tokea ulipoishika DINI?

wa shukran.
__________________
Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuhu [align=right][/align]
abjad is offline   Reply With Quote
Old 08-18-2011, 06:27 PM   #4
Zainab
Expert Member
 
Zainab's Avatar
 
Join Date: Aug 2011
Posts: 42
Default

Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuh Ust. Rashid43 Ust. Tungamaa kwa majibu yenu.
Shukran Wa baarakallahu fiik na salaam nyingi kutoka kwangu.

Dua nimeinakili, nitatembea nayo nina imani itasaidia Inshallah. Pindi mpatapo la zaidi nitashukuru kulipata na nitalitekeleza, sambamba na kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kwa kila jambo.
Zainab is offline   Reply With Quote
Old 08-18-2011, 06:44 PM   #5
abjad
Master
 
abjad's Avatar
 
Join Date: Mar 2011
Posts: 2,998
Default

Quote:
Originally Posted by Zainab View Post
Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuh Ust. Rashid43 Ust. Tungamaa kwa majibu yenu.
Shukran Wa baarakallahu fiik na salaam nyingi kutoka kwangu.

Dua nimeinakili, nitatembea nayo nina imani itasaidia Inshallah. Pindi mpatapo la zaidi nitashukuru kulipata na nitalitekeleza, sambamba na kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kwa kila jambo.
nakuomba unijibu Je
matatizo hayo....ni toka pale uliposhika DINI?
__________________
Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuhu [align=right][/align]
abjad is offline   Reply With Quote
Old 08-18-2011, 07:51 PM   #6
Zainab
Expert Member
 
Zainab's Avatar
 
Join Date: Aug 2011
Posts: 42
Default

Asante. Matatizo yangu ni ya muda mrefu kabla hata sijaishika dini labda niseme kabla sijaanza kuswali maana dini naiabud kwa muda mrefu japo mengi sikuwa nayajua.
Zainab is offline   Reply With Quote
Old 08-18-2011, 08:19 PM   #7
abjad
Master
 
abjad's Avatar
 
Join Date: Mar 2011
Posts: 2,998
Question

Quote:
Originally Posted by Zainab View Post
Asante. Matatizo yangu ni ya muda mrefu kabla hata sijaishika dini labda niseme kabla sijaanza kuswali maana dini naiabud kwa muda mrefu japo mengi sikuwa nayajua.
asante:

sasa nakuomba uwe mukhlis katika baadhi ya maallumat nninayoyataka kwako
(faham kwamba wengi wanayafuata majadiliano haya)

(1)je baada kuanza kushika dini unahisi % ngapi matatizo yamekupungikia?

AU ndio vile vile !!
au yamezidi ?

(2) katika ukoo wako waliokuwa na maruhani na wewe ulikua huyapendi mambo hayo na huenda ukawa hata unawashtumu hao marohani kwamba ni waongo !!
(nijibu hili hapa...ndipo nna shaka napo)
__________________
Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuhu [align=right][/align]
abjad is offline   Reply With Quote
Old 08-19-2011, 09:26 AM   #8
Zainab
Expert Member
 
Zainab's Avatar
 
Join Date: Aug 2011
Posts: 42
Default

1. Tangu nianze kuswali (na kwa kweli si muda mrefu), nahisi kupata amani moyoni kwa kiwango fulani (sijui ni % ngani), na nafsi yangu sasa inaniambia kuwa mengi yanayonisibu yatakuwa mikononi mwa Muumba wetu kwa kuwa namsujudia. Hata hivyo hali ya wasiwasi bado ninayo.
2. Kwa kipindi cha maisha yangu nimekumbana na machungu mengi na ili kujituliza, nimeshashawishiwa kutafuta tiba kwa kusomewa dua mbalimbali nk. Dua ni muhimu sana kwa maisha ya binaadam, kwani yote ni kumuomba Mwenyezi Mungu. Lakini kwa bahati mbaya ama sijui nzuri, ninachoamini kwa anayenisomea dua ni kuruani tu, akiongeza na mambo mengine papo hapo nafsi yangu huwa haiamini tena anachokifanya na kumtoa kasoro kimoyomoyo. Ninapotoka hapo huwa sina imani tena na nilichosaidiwa, kwa kuwa sikumwamini msomaji. Hivyo kwa kifupi, siamini kabisa mambo ya maruhani, mashetani, majini. Nimeshawahi kuambiwa na ndugu zangu kuwa ‘huponi kwa kuwa huna imani’. Sijajua bado kama ni kweli, yote namuachia Mungu. Nadhani utaungana nami kuwa watoa tiba wako waongo wengi tu.
Zainab is offline   Reply With Quote
Old 08-19-2011, 11:44 AM   #9
Mkolon
Senior Expert Member
 
Mkolon's Avatar
 
Join Date: Dec 2010
Posts: 141
Default

Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuh
Kulikuwa na kipindi fulani nilikuwa napatwa na wasiwasi sana, nikamuuliza ostadhi akaniambia penda kulitaja mara kwa mara jina lolote la Allah, na ostadha mmoja akaniambia nilitaje 'YA RATIF' mara kwa mara.

Nikafanya hivyo mara kwa mara kila ninapohisi wasiwasi nawakati mwingine bila kuwa na wasiwasi, wasiwasi ukaondoka kabisa na sasa nipo huruu
Nakushauri penda kulitaja mara kwa mara Maika wa Allah huwa jirani na wewe unapotaja jina la Allah masheitwani wanaokutia wasiwasi watakukimbia.
Allah ahlam
Allahuma Sali Wa Saalim Alla Sayidina Muhammad (SAW)
Mkolon is offline   Reply With Quote
Old 08-19-2011, 12:32 PM   #10
Zainab
Expert Member
 
Zainab's Avatar
 
Join Date: Aug 2011
Posts: 42
Default

Shukran Wa baarakallahu fiik Ust. Mkolon.

Nina kijitabu cha '99 Names of Allah' natembea nacho na kuna baadhi ya majina huyataja mara kwa mara. Jina la 'YA-LATIF' linafafanuliwa hivi: Mwenye kutaja jina hili mara 133 kila siku, riziki yake itaongezeka na mambo yake yote yatamalizika kwa njia inayomridhisha.

Insha'Allah, nitaelekea katika jina hilo na kulitaja kadri niwezavyo. Kwa jinsi nilivyodhamiria, kila nitakaloelekezwa ambalo litakuwa ndani ya uwezo wangu nitalitekeleza kwa uwezo wake M'Mungu.

JUMAA MUBARAK/ R-DHAN KARIM.
Zainab is offline   Reply With Quote
Reply

Thread Tools Search this Thread
Search this Thread:

Advanced Search
Display Modes

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off

Forum Jump

Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
DAWA YA UGONJWA WA KISUKARI Salim Afya na tiba 8 07-31-2013 11:30 PM
Ugonjwa wa Sukari Diabetes mzizimkavu2009 Afya na tiba 1 08-14-2010 07:11 AM
Ugonjwa wa Moyo mzizimkavu2009 Afya na tiba 1 08-14-2010 07:08 AM
UGONJWA ULIMWENGUNI muwahid Uliza tafsiri za ndoto kwa Sheikh Rashid. 1 06-26-2010 05:45 PM
WASIWASI WA IBLIS Mordiy Ukumbi wa Dini 2 11-20-2008 07:05 PM


All times are GMT +4. The time now is 09:12 AM.

Powered by vBulletin® Version 3.8.3
Copyright ©2000 - 2016, Jelsoft Enterprises Ltd. Mahmoud Al-Asmi