Kimbunga chaua 91 Oklahoma

Kimbunga kikubwa kilichoukumba mji wa Oklahoma nchini Marekani kimeuwa watu 91 wakiwemo watoto 20. Maafa makubwa yametokea katika kitongoji cha Moore, ambacho kimepitiwa na upepo unaosafiri kwa kasi ya Km 300 kwa saa.

Rais wa Marekani Barrack Obama ameitangaza Oklahoma kuwa eneo la janga kubwa na kuagiza usaidizi zaidi kupelekwa katika eneo lililoathirika zaidi katika kitongoji cha Moore. Kimbunga hicho ndicho kikubwa zaidi kuikumba Marekani baada ya kile kilicholikumba eneo la Jouplin katika jimbo la Missouri miaka miwili iliyopita ambacho kiliuwa watu 166.

Maafisa wa uokozi wamekuwa wakitafuta manusura zaidi chini ya vifusi vya shule iliyoporomoka ya Plaza Towers ambayo imeathiriwa zaidi na kimbunga hicho.

Shule nyingine ya msingi ya Briarwood ,nyumba kadhaa na hospitali ni miongoni mwa majengo yaliyoangushwa na kuwaacha wakaazi wa mji huo wapatao 50,000 wakiwa wamegutushwa na janga hilo lililowaacha na msiba.

Maafa yaliyosababishwa na kimbunga Oklahoma

Maafa yaliyosababishwa na kimbunga Oklahoma

Afisa wa afya wa Oklahoma amesema 20 kati ya watu 91 waliopoteza maisha yao ni watoto.Afisi ya afya ya eneo hilo imethibitisha vifo hivyo na kuongeza kuwa idadi ya waathiriwa inatarajiwa kuongezeka.

Kimbunga chauharibu sana mji wa Moore

Kati ya watu 240 waliojeruhiwa,60 kati yao ni watoto.Mtaa wa Moore umeharibiwa vibaya huku kukishuhudiwa uharibifu mkubwa wa mali na miundo mbinu na magari yaliyoharibiwa yakiwa yamerundikana.

Gavana wa jimbo hilo la Oklahoma Mary Fallin amesema leo ni siku ya huzuni kwa wakaazi wa eneo hilo.

Huku waokoaji wakiwa bado wanaendelea kutafuta manusura, taasisi za tahadhari ya vimbunga zinaonya kuwa majimbo mengine huenda pia yakakumbwa na kimbunga hicho, likiwemo Texas na mengine yaliyo kusini mwa nchi hiyo.

Kimbunga Marekani

Kimbunga Marekani

Shirika la kitaifa la utabiri wa hali ya hewa limeorodhesha kimbunga hicho kwa kiwango cha EF4 kwenye kipimo cha Fujita hii ikimaanisha kuwa kiko katika daraja la pili la vimbunga vikali vinavyoandamana na upepo  unaovuma kwa kasi ya kilomita 320 kwa saa.

Ilani yatolewa muda mfupi kabla ya kimbunga kufika

Kituo cha kutabiri vimbunga kilitoa ilani ya mji huo wa Oklahoma kukumbwa na kimbunga dakika 16 kabla kimbunga hicho kuharibu mji huo.Mkaazi mmoja wa eneo hilo anasema muda huo ulikuwa mfupi kwa wao kukimbilia maeneo salama.

Shirika la kusimamia viwanja vya ndege limeahirisha kwa muda usafiri wa ndege katika eneo hilo na kuruhusu tu zile zinazobeba misaada kwa ajili ya waathiriwa wa eneo hilo.

Huu ni msimu wa vimbunga na vimbunga zaidi vimetabiriwa.Jumapili iliyopita vimbunga viliwauawa watu wawili na kuwajeruhi wengine 39 mjini Oklahoma.

Kulingana na maelezo ya walioshuhudia kimbunga cha usiku wa kuamkia leo,kimbunga hicho kilikuwa kikali kushinda cha mwaka 1999 ambacho kinadiriwa kuwa cha tatu kibaya zaidi katika historia ya Marekani kwani kiliharibu mali inayokisiwa kufikia dola bilioni 1 wakati huo.Vimbunga vya Joplin na Tuscaloosa vilivokumba Marekani mwaka 2011 vinaorodheshwa pia kuwa viliiletea nchi hiyo hasara kubwa.

Source: DW

Jinsi ya kumfurahisha mumeo

1- Mapokezi mazuria)   Baada ya kurejea kutoka kazini, skuli, safarini, au popote  pale palipowatenganisha, anza kwa maamkizi mazuri.b)   Mpokee kwa uso mchangamfuc)     Jipambe na ujitie manukato (Perfume)d)    Anza na habari nzuri na chelewesha habari yoyote  mbaya mpaka atapokwisha pumzikae)     Mpokee kwa maneno ya mapenzi na hamu/shaukuf)     Fanya jitihada kubwa katikaMN mapishi mazuri na  kitayarishe kwa wakati.

2-  Ipambe na ilainishe sautia)   Ni kwa ajili ya mumeo peke yake, isitumike mbele ya wanaume wasio mahram (wanaume wanaoweza     kukuoa iwapo utakuwa huna mume)

3-  Harufu nzuri na kujipamba mwilia)      Ushughulikie vyema mwili wako na afya yako.b)      Vaa nguo za kuvutia na jitie manukato.c)     Koga mara kwa mara, na baada ya siku za hedhi, safisha  madoa madoa yote ya damu na ondosha  harufu mbaya.d)    Jiepushe kuonekana na mumeo ukiwa na nguo chafu au ukiwa ovyo.e)    Jiepushe na mapambo yaliyokatazwa, mfano wa tattoo.(kuchorwa mwili kwa kitu cha moto kwa ajili ya pambo.)f)      Tumia aina ya manukano, rangi, na nguo ambazo mumeo anazipenda.g)    Badilisha mtindo wa nywele, manukato n.k. mara kwa mara.h)    Hata hivyo usifanye isirafu katika vitu hivi, na bila shaka fanya hivyo mbele ya mahram zako na wanawake wenzako tu.

4- Jimai (Tendo la ndoa)a)      Harakisha kufanya jimai pale mumeo anapokuwa na hamu ya tendohilo.b)   Weka mwili wako safi na wenye kunukia kadri iwezekanavyo pamoja na kujisafisha maji maji yanayotoka wakati wa jimai.c)     Semeshaneni maneno ya mapenzi na mumeo.d)    Mwachie mumeo atosheleze kabisa hamu yake.e)    Chagua wakati muwafaka na muda mzuri wa kumchangamsha mumeo, na kumtia hamu ya kufanya jimai, mfano baada ya kurudi safari, mwisho wa wiki, n.k.

5-  Kutosheka na kile ulichojaaliwa na Allaah (S.W.T.)a)   Usiwe mnyonge kwa kuwa mumeo ni maskini au na aina ya kazi  anayofanya.b)    Uwaangalie masikini, wagonjwa, na vilema na kumkumbuka Allaah (S.W.T.) kwa yote yale uliyopewa.c)   Ni lazima ukumbuke kuwa utajiri wa kweli upo katika Iman na ucha Mungu

       6- Kutoshughulishwa na mambo ya kidunia          a)    Usiichukulie dunia hii kuwa ya matumaini na kushughulishwa nayo.b)    Usimdai mumeo vitu vingi visivyo na ulazima.c)    Kutosheka na kuishi maisha ya kawaida hakuna maana ya kutofurahia/kutotumia kilicho kizuri na kilichoruhusiwa (halali), bali kunamaanisha mtu kuangalia akhera yake na kutumia kile ambacho Allaah Amempa kwa ajili ya kupata Pepo (Jannah).d)    Muhimize mumeo kupunguza matumizi na kubakisha fedha kwa ajili ya kutoa sadaka na kuwalisha masikini na wasiojiweza

7- Shukurania)    Kutokana na hadithi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wengi wa watu wa motoni ni wanawake kwa sababu hawana shukurani na kutoridhia wema wanaofanyiwa.b)   Matokeo ya kuwa na shukurani ni kuwa mumeo atakupenda zaidi na atafanya awezalo kukufurahisha kwa njia nyingi.c)    Matokeo ya kutokuwa na shukurani ni kuwa mumeo atavunjika moyo na ataanza kujiuliza: Kwa nini nilazimike kumfanyia wema hali ya kuwa hana shukurani?

8- Kujitolea na Twaaa)    Hususan nyakati za maharibiko/matatizo makubwa katika mwili wa mumeo au katika kazi yake, mfano  ajali au kufilisika.b)   Kumpa msaada kwa kufanya kazi,  msaada wa fedha, na vitu vyengine iwapo utahitajika.

8- Kujitolea na Twaaa)    Hususan nyakati za maharibiko/matatizo makubwa katika mwili wa mumeo au katika kazi yake, mfano  ajali au kufilisika.b)  

9- Kumtiia)    Kumtii katika yote anayokuamrisha, isipokuwa katika yale  yaliyoharamishwa.b)   Katika Uislam, mume ndie kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na mshauri wake.

10- Kumliwaza anapokasirika a)   Kwanza kabisa, jaribu kujiepusha na kile ambacho una uhakika kuwa kitamkasirisha.b)   Bali iwapo imetokezea kuwa huwezi, basi jaribu kuepusha ugomvi kwa njia zifuatazo:      1.    Iwapo wewe ndiye uliyekosea, basi mtake radhi (muombe msamaha)      2.     Iwapo yeye ndiye aliyekosea basi:-    Endelea kunyamaza badala ya kubishana au-     Samehe haki yako au-     Subiri hadi zitakapokwisha hasira zake na mlijadilisuala hilo kwa    amani3.    Iwapo amekasirishwa na mambo nje ya nyumba basi:           -    Endelea kunyamaza kimya hadi hasira zakezitapokwisha                     -       Mpe udhuru (wa hasira zake), mfano kuchoka, matatizo kazini, kuna mtu amemuudhi.-   Usimuulize masuala mengi na kushikilia kujua nini kimetokezea, mfano (kumwambia) (1) Ni lazima unieleze nini kimetokezea.  (2) Ni lazima nijue nini kimekukasirisha namna hiyo. (3) Unanificha kitu, na mimi nina haki ya kujua.

11- Muongozo (na majukumu) anapokuwa hayupo:a)      Jilinde na mahusiano yoyote yaliyokatazwa.b)    Zidhibiti siri za familia, hususan jimai (tendo la ndoa) na  mambo ambayo mumeo hapendi watu wengine wayajue.c)      Ishughulikie nyumba na watoto.d)      Ishughulikie mali yake na vitu vyake.e)      Usitoke nje ya nyumba yako bila ya ruhusa yake na bila ya hijaab iliyo kamili.f)       Usikaribishe watu ambao mumeo hapendi kuja kwao.g)      Usimruhusu mwanamme yeyote asie Mahram wako kuwa nawe faragha pahala popote.h)      Kuwa mwema kwa wazazi wake na jamaa zake akiwa hayupo.

12- Kuonyesha heshima kwa familia yake na rafiki zakea)   Ni lazima uwakaribishe wageni wake na ujaribu kuwafurahisha, hususan wazazi wake.b)   Ni lazima uepuke matatizo kati yako na jamaa zake kwa kadri iwezekanavyo.c)   Ni lazima uepuke kumuweka pahala ambapo inambidi  achague kati ya mama yake na mkewe.d)  Onyesha urafiki (makaribisho mazuri) kwa wageni wake kwa kuwatayarishia pahala pazuri pa kuketi, chakula kizuri, kuwakaribisha vizuri wake zao, n.k.e)   Muhimize kuwatembelea jamaa zake na uwaalike nyumbani kwako.f)   Wapigie simu wazazi na dada zake, watumie barua, na wanunulie zawadi, wasaidie wakati wanapoharibikiwa, n.k.

13- Wivu wenye kukubalikaa)     Wivu ni aina ya mapenzi ya mke kwa mumewe bali ni lazima ubakie katika mipaka ya Uislam, mfano  kutowatukana na kuwasengenya wengine, kuwavunjia heshima zao, n.k.b)      Usifuate au kuanzisha tuhuma zisizo na msingi

14- Subira na kumpa moyoa)      Kuwa na subira mnapokabiliwa na umasikini na hali ngumu (kimaisha  na kifamilia).b)    Wakati mnapokabiliwa na majanga na maharibiko ambayo yanaweza kutokea kwako, kwa mumeo, kwa watoto wako, jamaa au mali, mfano magonjwa, ajali, kifo, n.k.c)    Wakati mnapokabiliwa na matatizo katika Da’wah (kufungwa jela, kukamatwa, n.k.), kuwa na subira na mhimize katika kubaki katika njia ya Allaah na kumkumbusha kuhusu Pepo.d)    Anapokufanyia uovu, mlipe uovu wake kwa kumfanyia wema.

15- Msaidie katika kumtii Allaah, Da’awah (Ulinganiaji) na Jihaada)      Shirikiana na mumeo na mkumbushe ibada mbali mbali za   faradhi na za Sunnah.b)     Muhimize kusali usiku.c)    Sikiliza na soma Qur-aan peke yako na ukiwa pamoja na mumeo.d)    Mkumbuke (mtaje) Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) sana, hasa hasa baada ya Alfajiri na kabla ya Magharibi.e)   Pangeni pamoja shughuli za Da’wah kwa wanawake na  watoto.f)     Jifunze hukumu za Kiislam na adabu za Kiislam kwa wanawake.g)    Msaidie mumeo katika shughuli zake kwa kumhimiza, kumpa ushauri mwema, kumliwaza machungu yake, n.k.h)      Samehe baadhi ya haki zako na samehe sehemu ya muda wako wa kuwa pamoja na mumeo kwa ajili ya Da’wah.i)      Mhimize kwenda Jihad anapohitajika na mkumbushe kuwa wewe na watoto mtakuwa katika hifadhi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). 

16. Utunzaji mzuri wa Nyumbaa)   Iweke nyumba safi, weka mapambo na iweke katika mpangilio mzuri.b)    Badilisha mpangilio wa nyumba mara kwa mara ili kuzuia kupoteza hamu nayo na kuchoshwa nayo.c)    Tayarisha chakula kizuri na chenye afya.d)   Jifunze ujuzi wowote wa muhimu kuhusu uangalizi wa nyumba, mfano kushona, n.k.e)   Jifunze namna ya kuwalea vyema watoto na kwa njia ya Kiislam. 

17- Kuhifadhi/Kutunza fedha na familiaa)   Usitumie fedha zake, hata kwa sadaka bila ya ruhusa yake labda uwe na uhakika kuwa atakubaliana na matumizi hayo.b)   Ilinde nyumba yake, gari, n.k. anapokuwa hayupo.c)    Waweke watoto katika hali nzuri, nguo safi, n.k. Zingatia lishe yao, afya, elimu, tabia, n.k wafunze Uislam na wahadithie visa vya Mitume (‘Alayhimus Salaam) na Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum).

86 Kafara ya kikao

(196)

سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك

“Subhaanaka Allahumma Wa Bihamdika, Ash-hadu Alla Ilaaha Illa Anta Astaghfiruka Wa Atuwbu Ilayka”“Kutakasika ni Kwako ewe Mwenyezi Mungu  na sifa njema zote ni Zako.  Nakiri kwamba hakuna mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, nakuomba msamaha na ninarejea Kwako”

Hadith

Kutoka kwa Abu Dharr Al-Ghifariy رضي الله عنه   naye kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم  akisimulia yale aliyopokea kutoka kwa  Bwana wake   عَزَّ وَجَلَّ   ni:

Enyi waja Wangu, Nimeikataza nafsi Yangu dhulma na Nimeiharamisha kwenu (hiyo dhulma), kwa hivyo msidhulumiane.

Enyi waja Wangu, nyote mumepotea isipokuwa wale Niliowaongoza, kwa hivyo tafuteni muongozo kutoka Kwangu Nitakuongozeni.

Enyi waja Wangu nyote mna njaa isipokuwa wale Niliowalisha, kwa hivyo tafuteni chakula kutoka Kwangu na Nitakulisheni.

Enyi waja Wangu, nyote muko uchi isipokuwa wale niliowavika nguo, kwa hivyo tafuteni vazi kutoka Kwangu nitakuvisheni.

Enyi waja Wangu, mnafanya  makosa usiku na mchana, na ninasamehe dhambi zote, kwa hivyo tafuteni msamaha kutoka Kwangu nitakusameheni.

Enyi waja Wangu hamuwezi kunidhuru Mimi wala kuninufaisha. 

Enyi waja Wangu, ingekuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mcha Mungu kama moyo wa mcha Mungu yeyote katika nyinyi, haitaongeza  chochote katika ufalme Wangu.

Enyi waja Wangu, angelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mbaya kama moyo mbaya wa mtu miongoni mwenu (mtu mbaya kupita kiasi) haitonipunguzia chochote katika ufalme Wangu.

Enyi  waja Wangu ingelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi mukasimama pahala pamoja na mkaniomba, na nikawapa kila mmoja alichoomba, haitonipunguzia katika nilicho nacho zaidi kuliko sindano inavyopunguza bahari inapochovya.

Enyi waja Wangu, ni vitendo vyenu ninavyovihesabu, kwa ajili yenu nikakulipeni.  Kwa hivyo anayekuta wema amshukuru Allaah na yule anayekuta yasiokuwa mema (basi) ajilaumu mwenyewe.

Imesimuliwa na Muslim

Utalipwa kwa vitendo vyako

Kasema Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

“Amenijia Jibriyl akasema: Ewe Muhammad ishi upendavyo bila shaka wewe ni maiti (utakufa), na mpende umtakaye bila shaka utafarikiana naye, na tenda unavyopenda lakini ujue utalipwa kwa vitendo hivyo, na tambua kwamba utukufu wa Muumin ni Qiyaamul-Llayl, na heshima yake ni kujitosheleza Na watu”

[Al Haakim na Al Bayhaqiy, na Al Mundhiriy na Al-Abaaniy wamesema ni Hadiyth Hasan]