Hadith

Kutoka kwa Ibnu Mas-uud Al-Ansary radhia Allahu anhu amesema : Amesema Mtume (swalla Allahu alayhi wasallam): “Atakaesoma usiku aya mbili za mwisho za Suratul Baqarah basi zitamtosheleza.”(Bukhari na Muslim)

Amesema Imam Nawawy Rahimahu Allah “Kumtosheleza maana yake ni: Ima Kumtosheleza na kisimamo cha usiku, au kumtosheleza kutokana na vitimbi vya shetani au kumtosheleza na mabalaa mengine au inakusanya yote hayo.

Katika dua zako za usiku usisahau aya 2 za mwisho za Suratul Baqarah. Kama huzijui jifunze na tuwafunze watoto wetu.

Aya mbili za mwisho wa Suratul Baqarah ni hizi 👇

آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْهِ مِنْ رَبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِنْ رُسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ

Maana yake:  ‘Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet’ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.’

لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِنْ نَسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنْتَ مَوْلَانَا فَانْصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ

Maana yake: ‘Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni:) Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri.’

Umoja wetu ni nguvu yetu

image

Kimsingi maana ya umoja na mshikamano kati ya Waislamu si kuwataka wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu kutupilia mbali itikadi zao, bali lengo kuu ni kujenga maelewano na mshikamano mbele ya adui wao wa pamoja. Naam, tofauti hizo za kimadhehebu zinaweza kujadiliwa kwa njia za kimantiki na busara katika vikao vya mijadala ya kielimu vya wanazuoni na maulamaa wa Kiislamu na kufikia nukta za wazi. Hapana shaka kuwa makelele na malumbano yasiyokuwa ya kielimu katika vikao vya umma kuhusu masuala ya kitaalamu hayawezi kuwa na matunda ya kuridhisha. Tunaweza kusema hapa kuwa moja ya vizuizi vya umoja na mshikamano katika umma ni kutolewa mijadala kama hiyo ya kielimu na kitaalamu kuhusu masuala ambao Waislamu wanatofautiana juu yake katika vikao vya umma na kwa njia ya kichochezi.

Dini tukufu ya Kiislamu inawalingania wafuasi wake wote kutumia akili na kutafakari na kuzidisha maarifa na elimu yao kadiri inavyowezekana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, kuwa na maarifa na elimu huzuia mifarakano na ukosefu wa maelewano. Inasikitisha kuona kwamba katika zama za sasa za mawqasiliano na utandawazi Waislamu wa madhehebu moja hawajui kabisa au wana maarifa finyu kuhusu itikadi za ndugu zao wa madhehebu nyingine ya Kiislamu. Upungufu huu wa maarifa kuhusu itikadi za madhehebu tofauti za Kiislamu umekuwa moja ya vizuizi vya umoja na mshikamano wa Kiislamu na umekuwa ukisababisha mambo mengi ya kusikitisha katika ulimwengu wa Kiislamu.

Mwanafikra mmoja wa Kiislamu anasema: “Tishio linalowakabili Waislamu kutokana na hali ya kutofahamiana na kudhaniana vibaya ni kubwa zaidi kuliko lile linalotokana na tofauti zao za kimadhehebu.”

Mwingine anasema kuhusu taathira mbaya za kutofahamiana kati ya Waislamu na mchango wake katika kukuza hitilafu kwamba: “Tofauti za kimadhehebu na kiitikadi ni jambo ambalo limekuwepo katika zama zote lakini jambo linalobadilika kila wakati na katika kila zama ni ukosefu wa maelewano na kutofahamiana kwa pande husika. Kwa sababu hiyo, moto wa ugomvi, malumbano na mifarakano huchochewa zaidi na zaidi.”

Sheikh Muhammad Abu Zahra ambaye alikuwa miongoni mwa maulamaa wa chuo cha al Azhar cha Misri amesema:
“Tofauti na hitilafu zilizoko kati ya Waislamu zimepenya na kuingia zaidi katika fikra, hisia na nyoyo zao kutokana na taasubi na chuki za kikaumu na kimadhehebu kwa kadiri kwamba Muislamu mmoja humuangalia Muislamu mwenzake anayehitilafiana naye kifikra kama adui aliyeko mafichoni dhidi yake na si kama mtu mwenye mitazamo tofauti kama yeye anayefanya jitihada za kujua hakika ya sheria za Mwenyezi Mungu.”

 
Amkeni wapendwa waislamu

umoja wetu ni nguvu yetu

Imeandikwa na Sheikh Rashid Ashukery.

Kitabu chako!

image

KUPANDISHWA MATENDO KWA ALLAH SUBHANAH

Amesema Allah (Subhanahu wataala) “Na hakika juu yenu kuna wenye kuwatunza” “Watukufu wenye kundika(11)Wanayajua yote mnayoyatenda(12)” [Suratul Infitwaar]

Tumeona kua, kila mmoja anapotamka tamko au kufanya lolote lile, hakika malaika wanamjazia katika kitabu chake.
Na malaika wanampelekea nani? Wanampelekea Allah(subhanahu wataala).

Je ulishawahi kujiuliza ni yapi ambayo yameandikwa kwenye kitabu chako? Je ulishawahi kujiuliza ni yapi ambayo amepelekwa Allah (subhanahu wataala)?

Ikiwa mzee wako,mke wako,mume wako au boss wako wa kazini hutaki apewe ripoti chafu au juu ya maovu yako. Sasa vipi kwa Allah (subhanahu wataala) alietukuka?

Tunamuomba Allah aturuzuku kumuonea haya. Kwani mangapi yetu yameandikwa ambayo hatukubali wala haturidhiki kupelekwa kwa Allah. Lakini tunamuomba Allah ambae ametustiri atusamehe. Kwani Mola wangu ni mwingi wa msamaha na mwenye kurehemu

DR. Zakir Naik

DR. ZAKIR NAIK WINS KING FAISAL AWARD 2015

Sekenke Web extends its heartfelt congratulations to DR. ZAKIR NAIK who was conferred the prestigious “37TH KING FAISAL INTERNATIONAL PRIZE 2015” for ‘SERVICE TO ISLAM’, Alhamdulillah, as announced by Makkah Governer Prince Khaled Al-Faisal (Director General) and Abdullah Al-Othaimeen (Secretary-General) of the King Faisal Foundation at a glittering function in Riyadh on 3rd Feb. 2015. The King Faisal Award given for the category ‘Service to Islam’ is the most recognized and prestigious Award in the Muslim World, similar to the ‘Noble Prize’. Dr. Zakir Naik is the 2nd Indian to be conferred this Award after Maulana Shaikh Sayyid Abul-Hasan Ali Al-Hasani Al-Nadawi who shared this Award with Dr. Mohammad Natsir of Indonesia in 1980. The Award Ceremony will be held under the auspices of King Salman Bin Abdul Aziz, InshaAllah, sometime in the first week of March 2015, at Prince Sultan Grand Hall, Faisaliah Center, Riyadh, Saudi Arabia. This KING FAISAL INTERNATIONAL PRIZE is an annual award conferred on “dedicated men and women with exceptional achievements in five categories – Service to Islam, Islamic Studies, Arabic Literature and Language, Science and Medicine – and whose contributions make a positive difference” globally. Attached alongwith are a few media articles and website links for your kind information. The extended list may be downloaded from http://www.irf.net/space/DZN_Faisal_Award.rar

Ajali 11 mbaya sana

Hizi ndio ajali mbaya kuliko zote hapa Duniani.

Japo wengi huziona za kawaida tu, omba usikutane nazo kabisa!

1. Kuvunjika Moyo wa Kuswali
2. Kutopenda kusikiliza mawaidha
3. Kutojali halali na haramu
4. Kutosoma QUR-AN
5. Kuondokewa na hofu ya Mungu
6. Kutowajali wazazi
7. Kutokuwa na huruma kwa viumbe wa Mwenyezi Mungu
8. Kutenda Dhambi wakati unajua  
9. Kudhani utaishi milele
10. Kutokua na Roho ya Kusamehe.
11. Kubwa zaidi ya yote ni Shirk (kumshirikisha Mwenyezi Mungu).

Namuomba Mwenyezi Mungu atuepushe na ajali hizo.

Ameen.